Jumapili 28 Septemba 2025 - 22:05
Mpango wa Siri wa Shetani

Hawzah/ Je, ni kwa jinsi gani muumini mwenye kusali anaweza taratibu kubadilika na kuwa mtu mwenye kughafilika? Mpango wa siri wa Iblisi huanza kwa kushambulia swala ya usiku na kuishia katika kuuteka kikamilifu moyo; mpango ambao kuutambua kwake kunaweza kuwa njia ya wokovu.

Shirika la Habari la Hawza - Umri wa mwanadamu unapaswa kutumika katika ibada na uchaji Mungu, Mja wa kweli daima huogopa kutengana na Mola wake; na ndiyo maana Imam Zayn al-‘Abidin (a.s.) akimuelekea Mwenyezi Mungu Mtukufu husema hivi:

 1  (اللَّهُمَّ ... عَمِّرْنی ما کانَ‌ عُمری‌ بِذْلَةً فی طاعَتِکَ، فإذا کانَ عُمری مَرتَعاً لِلشَّیطانِ فَاقبِضْنی إلَیکَ)

Ewe Mwenyezi Mungu! Kadiri ambavyo umri wangu unatumika katika ibada na uja kwako, nibarikie umri na unifanyie urefu wa maisha, lakini pindi umri wangu utakapo geuka kuwa malisho ya shetani, ichukue roho yangu.

Sherehe:
Mwenye kupenda kwa kweli na kwa dhati hawezi kustahimili hata kidogo kutengana na mpenzi wake. Haukubali ulimwengu bila ya mpenzi wake, ulimwengu bila ya mpenzi katika macho ya mpenzi wa kweli huonekana wa giza na wa kuchukiza, mpenzi huyo huchukia kila kitu kinachoweza kumsogeza mbali na mpenzi wake.

Hakika Imam Zayn al-‘Abidin (a.s.) katika kifungu hiki kizuri mno tena cha mapenzi makubwa anatufundisha njia na mwongozo wa kufikia furaha ya milele. Kwamba inatupasa kwa namna hii kumuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu ili tufikie furaha ya milele.

Ewe Mungu! Kadiri ninapovaa vazi la uja na utiifu kwako, nipe nafasi ya kuishi na kuvuta pumzi, lakini pindi tu utakaposhuhudia umri wangu na maisha yangu vimekuwa uwanja wa shetani, chukua roho yangu. Mimi sitaki pumzi yoyote ambayo si katika utiifu kwako; na huu ndio upeo wa mapenzi na kujitoa mhanga kwa mpenzi.

Lakini je, vipi umri wa muumini unaweza kugeuka kuwa malisho ya shetani?

Jambo lililo dhahiri ni kwamba shetani daima hukaa akivizia, na humjia kila mtu kupitia mlango unaomfaa yeye.

Siku moja, shetani hufanya swala ya usiku ionekane haina umuhimu machoni mwa mtu.

Siku nyingine, humchelewesha mtu asiswali katika wakati wa mwanzo.

Katika hatua inayofuata, humnyang’anya utamu na raha ya swala.

Anapomnyang'anya swala, huelekea hatua nyingine zaidi.

Hijabu pungufu, kuzama katika mitandao ya kijamii, kutazama filamu zisizo na maadili, kutokuwa makini katika kupata mali halali, kusengenya, kutuhumu, kutowaheshimu baba na mama, kupuuza mahitaji ya wenye kuhitajia na mengineyo; hadi inapofikia yule muumini anapojitazama hujikuta kuwa kila kitu alichokuwa nacho, kila rasilimali ya kimaumbile aliyopewa, kila kiunganisho cha mapenzi kati yake na Mpenzi wake, vyote vimepotea, na mwili wake mzima umepoteza nuru ya Mwenyezi Mungu na umegeuka kuwa uwanja wa shetani.

Na kwa sababu hiyo, Mwenyezi Mungu mara kwa mara katika Qur’ani anasema:

 2  (وَلَا تَتَّبِعُوا خُطُوَاتِ الشَّیْطَانِ إِنَّهُ لَکُمْ عَدُوٌّ مُبِینٌ)

“Wala msifuate nyayo za shetani, hakika yeye ni adui yenu wa wazi kabisa.”

Rejea:

1. Dua ya ishirini, Sahifa Sajjadiyya.
2. Surat an-Nur, aya ya 21.

Imeandaliwa na kitengo cha Elimu na Utamaduni cha Shirika la Habari la Hawza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha